BETWAY NDIYO MDHAMINI MKUU WA SIMBA SC KWA MIAKA MITATU
Klabu ya mpira wa miguu nchini Tanzania, Simba Sports Club imepata
mdhamini mkuu mpya, ambapo mdhamini hiyo ni kampuni ya kubashiri ifahamikayo kwa
jina la BetWay
Aidha kampuni hiyo ya kubashiri imeingia mkataba wa kuwa
mdhamini mkuu wa club hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu yaani kuanzia msimu wa
2025/26 mpaka msimu wa 2027/28
Hii ni baada ya kampuni ya M-bet ambayo ilikuwa mdhamini wa
Simba kuanzia 2022 kusitisha mkataba na club hiyo namba tano kwa ubora barani
Afrika.
Hata hivyo hapo awali, kampuni ya M bet iliingia mkataba wa
miaka mitano kuidhamini timu ya simba kwa kuanzia 2022 mpaka 2026 lakini
wameshindwana na kuamua kujiweka pembeni.
MDHAMINI MPYA
Betway wameingia mkataba wa miaka mitatu na club ya simba na
sasa rasmi, simba atakuwa akivalia jezi zenye nembo ya Betway kifuani kuanzia
msimu huu 2025/26 mpaka pale kampuni hiyo itakapoachia ngazi ya udhamini ukuu.
Vile vile Kampuni imeweka kiasi cha sh Bilioni 20 za
kitanzania kwa miaka yote mitatu lakini zikilipwa kwa awamu tatu kwa kila msimu
Pia kampuni na club zimekubaliana kwamba kutakuwa na bonasi
mbali mbali zitakazotolewa na mdhamini huyo pindi timu itakapofanya vyema
kwenye mashindano, bonas hiyo itategemea na mafanikio ya club.
Licha ya kuwa mdhamini mkuu, lakini Betway hatoizuia club ya
simba kuwa na wadhamini wengine, ikiwa ni pamoja na matangazo ya biashara za Mo
Dewji ambazo zinamilikiwa na muwekezaji Mohamed Dewji mwenye hisa asilimia 49
ndani ya club hiyo.



Hakuna maoni