Zimbwe Jr ni mali ya Yanga akitokea Simba Sc
Club ya Young Africans wameendelea kuwaumiza mashabiki wa watani wao Simba SC baada ya kuendelea pale walipoishia,
Hii ni baada ya kupiga kwenye mshono, kwani msimu wa 2024/25 timu hiyo kongwe zaidi nchini Tanzania ilifanikiwa kunasa saini ya sukari ya wanasimba, Cloutus Chota Chama na kumsajili ikiwa bado alikuwa mchezaji pendwa katika club hiyo ya simba
Kuelekea msimu wa 2025/26, wameendelea kuwaumiza baada ya kunasa tena saini ya beki wa kushoto wa timu hiyo hiyo ya simba ambao ni watani wa jadi, Mohamed Hussein anayefahamika pia kwa jina la Zimbwe Junior.
Saa sita usiku wa kuamkia tarehe 6/8/2025 yanga walimtangaza Zimbwe kama mchezaji wao mpya baada ya kuinasa saini
sio suala geni kwa timu hizo mbili kuibiana wachezaji, hivyo msimu wa 2025/26 Mohamed Hussein atakuwa mchezaji wa club ya Yanga.
Translate to english


Hakuna maoni