FEISAL SALUM (FEI TOTO) KUTIMKIA SIMBA SC

 


Mkuu wa idara ya mawasiliano wa Azam Football Club, Thabith Chumwi Zakaria maarufu kama ZAKA ZAKAZI ameweka wazi kwamba Club ya Simba haina uwezo wa kiuchumi wa kuweza kumsajili mchezaji Feisal Salum "Fei Toto"

Feisal Salum ni mchezaji wa Azam FC aliyojiunga tangu mwaka 2023 akitokea katika club kongwe zaidi nchini tanzania Dar es Salaam Young aFRICANS sports club (Yanga). Licha ya kuwepo kwa tetesi nyingi za kumuhusisha mchezaji huyo either arudi yanga au ajiunge na simba.

ikumbukwe kwamba Simba SC na Yanga ni wapinzani wa siku zote tangu ligi ianzwe, kwa kiswahili wanaitwa WATANI WA JADI kwani ndio wanaunda Dabi ya Kariakoo na ndio dabi yenye nguvu zaidi mashariki mwa afrika

hivyo kutokana na kwamba YANGA ndio timu iliyomfanya feisal kuwa maarufu, basi simba wangelitamani kumsajili ili kumkomoa mpinzani wake, kama wanavyofanya siku zote kuibiana wachezaji

kwa namna feisal alivyoondoka yanga, imekuwa ni ngumu kuaminisha watu kwamba angeliweza kurudi tena kwani aliondoka kwa mshike mshike huku wakitupiana maneno na viongozi wa timu hiyo kwani alitaka kuvunja mkataba kinyume na utaratibu hali iliyofanya asiondoke kwa heri

hata hivyo baadaye viongozi wa yanga walikutana na viongozi wa azam na kuingia makubaliano ya kuuziana mchezaji huyo, lakini feisal alidai ameondoka kwa sababu ya maslahi kwani yanga alikuwa analipwa mshahara mdogo kulinganisha na alioahidiwa kuupata azam fc

hivyo hali hii ilipelekea watu wengi kuamini hatoweza kurudi yanga kwani ni maneno mengi walitupiana kipindi cha uhamisho wake kwenda azam fc

kueelekea msimu huu wa 205/26 katika usajili feisal amekuwa akihusishwa na mengi sana, aidha yanga wakiamini anaweza kurudi yanga, huku mashabiki wa simba wakidai ataenda simba.

basi vyanzo vyetu vilivyofuatilia viligundua kuwa mchezaji feisal hana ratiba ya kuondoka azam fc kujiunga na club mbili hizo zilizotajwa hapo juu

baada ya thabith chumwi zakaria ambaye ni Head of Information and Communication

Azam Football Club kuhojiwa kuhusu sakata hili la Feisal kutimkia Simba, aliweza kusema maneno haya

"Simba SC hawana pesa inayotosha kumnunua Feisal kutoka azam kwani, kipindi yanga na azam wanafanya makubaliano ya kuuziana mchezaji huyo basi yanga waliweka kipengele kwamba ejapo azam wakitaka kumuuza mchezaji huyo kwenda simba SC basi watapaswa kulipa kiasi cha Tsh 1000,000,000/= (shilingi bilioni moja) kwa Yanga"

hivyo kulingana na uchumi wa kawaida wa timu za tanzania, ni ngumu kwa timu kumsajili mchezaji kwa kiasi cha pesa hizo kwani ni nyingi sana, na kiafrika afrika zinaweza kusajili hadi wachezaji sita na sio mchezaji mmoja

thabith chumwi zakaria (zaka zakazi) aliendelea kusema kwamba itakuwa ni ngumu kwa sababu timu hiyo imeuzwa kwa bilioni 20 kwenda kwa muwekezaji Mohamed Dewji na hata wakishalipia kiasi hicho cha yanga, basi ikumbukwe kwamba watailipa azam pesa ya kumnunua mchezaji kutoka kwao kutokana na makubaliano yao, hivyo pesa itazidi kuwa nyingi zaidi.

ikumbukwe, nchini tanzania timu inayochukua kombe la ligi kuu inapata kiasi cha Tsh 600,000,000 (shilingi milioni mia sita tu za kitanzania) kama malipo ya bingwa. wa ligi

je itakuwa rahisi kwa timu kumsajili mchezaji mmoja kwa pesa nyingi zinazozidi karibia mara mbili ya pesa ya ubingwa"

BONYEZA HAPA KUONA WASIFU NA STATS ZA FEISAL SALUM

Translate this text to english


Hakuna maoni

Picha za mandhari zimetolewa na imagedepotpro. Inaendeshwa na Blogger.